2

Kumshinda Adui Mwili

Bwana Yesu Asifiwe!

Leo tutazungumza kidogo kuhusu eneo moja la vita vya kiroho ambalo ni lazima mtoto wa Mungu apigane kwa bidii na kushinda ili kuweza kufanikiwa kimaisha. Eneo hilo ni la kupigana na adui mwili. Ndiyo, nina maana mwili wako unaweza kuwa adui wako, nikimaanisha adui wa roho yako.

Tunasoma katika maandiko kuwa mtu ni roho, anayo nafsi, na anakaa katika mwili. Yaani maana yake ni kuwa mwili ni nyumba ambamo ndani yake inaishi roho yako wakati ukiwa hapa duniani. Ili roho yako iweze kuishi hapa duniani ni lazima ikae katika nyumba inayoitwa mwili.

Comments(2)

  1. Mgisa Ticha says:

    Somo tamu sanaaaaaaa ila umelikatisha. Tiririka zaidi mtumishi

  2. Ticha Mgisa says:

    Endelea kutuombea tu, Mungu azidi kutupa mafunuo mapya. Barikiwa