Mpendwa Mtu wa Mungu,

Huenda ungependa sana kumtumikia Mungu kwa njia mbalimbali lakini unakosa muda au ujuzi wa kufanya kile ambacho unataka kufanya kwa ajili ya Mungu. Usife moyo. Ukurasa huu unakupa fursa ya kumtumikia Mungu kwa kushirikiana na huduma hii ya Christ Rabbon Ministries. Unapotoa sadaka yako kwa ajili ya kuwezesha huduma hii ya kufundisha Injili ya Yesu Kristo kuwafikia watu wengi zaidi sehemu nyingi zaidi utakuwa umemtumikia Mungu kwa matoleo yako.

Kazi ya Mungu itawezekana kama wewe na mimi tunaoamini katika Injili ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo tutaiwezesha. Kazi ya kufundisha Injili ya Yesu Kristo ina gharama na inahitaji muda mwingi, vifaa, maombi, ujuzi na utaalamu, na raslimali fedha. Timu ya huduma ina mahitaji ya kibinadamu na kusafiri. Kutengeneza vitendea kazi vya kufundishia na kuhifadhi na kusambaza mafundisho pia ni gharama.

Bibilia inasema:
“Ni askari gani aendaye vitani wakati wowote kwa gharama zake mwenyewe?” (1Kor 9:7).

Basi ungana nasi katika kumtumikia Mungu kwa kuiwezesha kazi hii ya Mungu yenye baraka tele kwa kuchangia chochote kama ambavyo Roho wa Mungu atakugusa. Unaweza kuchangia kwa namna zifuatazo:

  • Kuweka fedha moja kwa moja kwenye akaunti ya huduma kwenye benki ya NBC na CRDB;
  • Kutuma sadaka yako kwa kutumia simu ya mkononi kwenye MPesa na TigoPesa;
  • Kununua audio CDs na video DVDs za mafundisho katika duka mtandao (Online Shop). Unaweza kuingia katika Duka Mtandao kwa kuchagua “Visit Online Shop” upande wa kulia kuangalia CDs na DVDs zilizopo. Kabla ya kununua ni lazima usajili akaunti kwa kubonyeza “Login/Create Account”.

Tunasoma katika bibilia:
“Kwa kuwa kila atakayeliitia Jina la Bwana ataokoka. Basi wamwiteje yeye wasiyemwamini? Tena wamwaminije yeye wasiyemsikia? Tena wamsikieje pasipo mhubiri? Tena wahubirije wasipopelekwa?” (Rum 10:13-15).

Kama ungependa kuiwezesha huduma hii kwa namna nyingine kama maombi, ujuzi, utaalamu, uimbaji, ushauri, nk, tafadhali wasiliana nasi kwa kubonyeza HAPA.